Karibu Fundi Kiganjani. Kwa kutumia mtandao huu, unakubaliana na vigezo na masharti yafuatayo:
Nafasi ya Mtandao: Fundi Kiganjani ni jukwaa la kidijitali linalounganisha wateja na mafundi wa kujitegemea. Sisi SIYO waajiri wa mafundi hawa, wala hatumiliki kampuni za ufundi.
Wajibu wa Mtumiaji: Unakubali kutoa taarifa za kweli wakati wa kujisajili (ikiwemo namba halali ya NIDA kwa mafundi). Taarifa za uongo zitasababisha kufungiwa kwa akaunti yako mara moja.
Malipo ya Kazi: Malipo yote ya huduma za ufundi yanafanyika moja kwa moja kati ya Mteja na Fundi. Fundi Kiganjani haihusiki na makato, upangaji wa bei, wala kudai madeni ya kazi zilizofanyika.
Kusitisha Huduma: Tunayo haki ya kusitisha, kufungia, au kufuta akaunti ya fundi au mteja yeyote atakayekiuka masharti, kutumia lugha za matusi, au kupata malalamiko mengi (Nyota mbaya) kutoka kwa watumiaji wengine.
Mabadiliko: Fundi Kiganjani inabaki na haki ya kubadilisha vigezo hivi wakati wowote.