Sera ya Faragha

Tunajali sana usalama wa taarifa zako binafsi kulingana na Sheria za Ulinzi wa Taarifa Binafsi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa Tunazokusanya: Tunakusanya majina yako, namba ya simu, barua pepe, namba ya NIDA (kwa mafundi), na taarifa za kijiografia (GPS Location) ili kurahisisha kukuunganisha na watu walio karibu nawe.

Matumizi ya Taarifa: Taarifa zako zinatumika kuboresha huduma zetu, kuunganisha wateja na mafundi, na kwa ajili ya usalama wa mtandao. Tunahifadhi rekodi za mawasiliano (Chat) ndani ya mfumo kwa ajili ya usuluhishi endapo kutatokea mgogoro.

Ulinzi wa Taarifa: Nenosiri (Password) lako limehifadhiwa kwa mfumo wa siri (Encrypted). Hatushiriki, hatuuzi, wala kusambaza taarifa zako kwa makampuni ya kibiashara.

Ushirikiano na Vyombo vya Dola: Taarifa zako zinaweza kutolewa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania endapo tu kutakuwa na hitaji la kisheria linalotambulika.