Ili kuwa na uzoefu mzuri na salama, tunashauri yafuatayo:
Kwa Wateja:
Tumia Mfumo wa Chat: Fanya makubaliano yote ya bei na aina ya kazi kupitia mfumo wetu wa Chat kabla ya kumpa kazi fundi. Hii inasaidia kuwa na ushahidi.
Kutanguliza Pesa: Epuka kumpa fundi pesa yote ya ufundi kabla kazi haijakamilika na wewe kuridhika, isipokuwa pesa ya kununulia vifaa vya kazi (ambayo unashauriwa kuyanunua mwenyewe au kwenda naye dukani).
Usalama Nyumbani: Kuwa makini unapomkaribisha mtu usiyemjua nyumbani kwako. Hakikisha kuna mtu mwingine wa karibu wakati kazi inafanyika.
Kwa Mafundi:
Kuwa Mtaalamu: Fika kwa wakati ulioahidi, na fanya kazi kwa weledi. Hii itakupa "Nyota 5" na kukuletea wateja wengi zaidi.
Ulinzi Wako: Toa makadirio (Quotation) ya wazi mapema ili kuepuka usumbufu wa mteja kukataa kulipa baada ya kazi.
Wasiliana: Tumia lugha nzuri kwa wateja kupitia mfumo wetu wa Chat.