Kanusho la Dhima

Tafadhali soma kwa umakini kanusho hili kabla ya kutumia huduma zetu:

Ubora wa Kazi: Fundi Kiganjani HAITOI dhamana (guarantee) ya ubora wa kazi itakayofanywa na fundi. Jukumu la kukagua kazi na kuridhika liko mikononi mwa mteja kabla ya kufanya malipo.

Uharibifu na Hasara: Fundi Kiganjani, wamiliki wake, na waendeshaji wake HAWATAHUSIKA na hasara yoyote, uharibifu wa mali, wizi, au majeraha yatakayotokea wakati fundi anatekeleza majukumu yake nyumbani au ofisini kwa mteja.

Utatuzi wa Migogoro: Migogoro yoyote ya kifedha au kiutendaji lazima itatuliwe kati ya Mteja na Fundi. Licha ya kwamba tunaweza kufungia akaunti ya mtumiaji mkorofi, hatutahusika kulipa fidia yoyote kwa niaba ya fundi au mteja.

Uthibitisho: Mteja anashauriwa kujiridhisha na utambulisho wa fundi pindi anapofika eneo la kazi kabla ya kumruhusu kuanza kazi.